22.11.13

Wednesday, November 20, 2013

(News) Mini ZIFF na Filamu za Bongo

MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake  (Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.
  Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
 
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena.

No comments: